.BAADA YA MUHONG KUJIUZULU ZITTO KABWE YAMPONGOZA

.BAADA YA MUHONG KUJIUZULU ZITTO KABWE YAMPONGOZA

1 ·
Nimepata taarifa kuwa Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Sospeter Muhongo amechukuwa hatua ya kujiuzulu katika nafasi hiyo. Napenda kuchukua nafasi hii kutambua busara aliyochukua ambayo naamini itasaidia harakati za kujenga demokrasia yenye uwajibikaji. Naamini uamuzi wa Ndugu Muhongo umewezesha kulinda heshima ya Bunge na maazimio yake. Kwa muda mfupi alioongoza Wizara hiyo, Ndugu Muhongo ameweza kuongoza mabadiliko kadhaa muhimu ya kiutendaji katika wizara hiyo na taasisi zake. Hata hivyo, nafasi ya Wizara aliyokuwa anaongoza katika suala la Tegeta Escrow imemtia doa kubwa ambalo ilikuwa lazima awajibike. Naamini Rais Kikwete atamteua mtu mchapakazi na makini zaidi atakayeweza kuendeleza yale mazuri ya Ndugu Muhongo na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza.
CCM wachinjana

CCM wachinjana


Na Kadama Malunde, Shinyanga
JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kunasa mtandao wa watu wanaojihusisha na vitendo vya mauaji, ukiwemo ule uliohusika na tukio la mauaji ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mwalugulu, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Daudi Lusalula Mbatiro (56).

Waliotajwa kuhusika katika mtandao huo ni pamoja na Diwani wa CCM Kata ya Mwalugulu wilayani Kahama, Bundala Kadilanha na mfanyabiashara wa Kagongwa, Tobo Mwanasana.
Wengine ambao wametajwa katika mtandao huo ni pamoja na Emmanuel Maziku, Masanja Shepa, Samwel Seni Budugu na Shija Shepa.
Katibu huyo wa CCM, Mbatiro aliuawa kwa kuchinjwa kama kuku Desemba 5, 2014.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, katika uchunguzi wa mauaji ya Mbatiro Jeshi hilo limewakamata watuhumiwa Emmanuel Maziku na Masanja Shepa na baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika na mauaji hayo.
Alisema baada ya kuwahoji watuhumiwa hao wawili, waliwataja wahusika wengine kuwa ni Diwani huyo wa CCM wa Mwalugulu, Bundala Kadilanha na mfanyabiashara Tobo Mwanasana.
Wengine waliotajwa ni Samweli Seni Budugu, mkazi wa Mwakitolyo na Shija Shepa, mkazi wa Mwalumba, Kahama.
Alisema awali Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa za watu hao liliweka mtego kwa kuwapigia simu ili kuwakodi kufanya mauaji katika Kijiji cha Nyindu na kufanikisha kuwakamata watu hao ambao hujihusisha na matukio mbalimbali ya mauaji.
Alisema baada ya kuwafanyia mahojiano watu hao wawili, walikiri kuhusika na matukio ya mauaji katika mikoa ya Shinyanga na Tabora kwa kukodiwa ili kuchinja watu kwa kisu na wao si kuwakata mapanga, ingawa wanaua vikongwe na kulipiza kisasi.
Kamanda Kamugisha alisema watuhumiwa walimtaja Samweli Seni Budugu kuwa ni kiongozi wao na wenzake ni Mwanasana, Kadila na Shepa na kwamba kabla ya mauaji hayo wanakwenda kupakwa dawa kwa waganga wao wa jadi ambao ni John Shija, mkazi wa Kijiji cha Lyabukande na mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Tabu, mkazi wa Kizungu.
Kamanda Kamugisha alisema watuhumiwa wote wamekiri kuhusika na matukio ya mauaji ya marehemu Ngolo Sakumi (69), mkazi wa Mwalugulu na walikodiwa kwa Sh 1,000,000, aliyewakodi ni Jikuba Kajile na Lukuba Nangi.
Tukio jingine walilokiri kuhusika ni mauaji ya Mary Seleman Masenya (45), mkazi wa Kijiji cha Matinje na walikodiwa kwa Sh 800,000 na wanawake watatu ambao ni wake wenza wa marehemu.
Alitaja tuko jingine walilohusika ni lile la mauaji ya Mboje Seni (70), mkazi wa Kijiji cha Butondo na walikodiwa kwa Sh 800,000 na Mwanabundi, mkazi wa Butondo na tukio jingine ni mauaji ya Kwigema Lubinza (60), mkazi wa Kijiji cha Kakulu, Kata ya Nyahanga.
Kamanda huyo alisema Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwakamata wahusika wengine wa matukio hayo, ikiwa ni pamoja na waganga wa kienyeji waliohusika, huku akiwataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika wote wa mauaji ya kukodiwa na mauaji ya vikongwe ili kukomesha tabia hiyo
 MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO LA UKONGA ATANGAZA KUJIUZULU PAMOJA WAJUMBE WOTE

MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO LA UKONGA ATANGAZA KUJIUZULU PAMOJA WAJUMBE WOTE

BW  THOMAS  NYAHENDE  AMBAYE  ALIKUWA  NI  MWENYEKITI   WA  JIMBO  LA  UKONGE

KAULI  YAKE  KUPITIA  UKARASA  WAKE  WA  FACEBOOK
· 
Makamanda na Marafiki zangu wote,
Napenda kuwafahamisha kuwa Jana Jumamosi tarehe 24 January 2015 nimetangaza rasmi kujiuzulu nafasi yangu ya Mwenyekiti Jimbo la UKONGA. Katika hali hiyo wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji Jimbo la UKONGA nao wamejiuzulu ili kuungana na Mwenyekiti wao.
Hatua hiyo ngumu sana tumeifikia jana baada ya kushauriana na Mwenyekiti wetu wa Taifa Kamanda Mbowe kufuatia hali ya sintofahamu iliyokuwepo kwa muda mrefu baina ya Viongozi wa Jimbo la UKONGA na Mratibu wa Kanda yetu ya Pwani. Tumefikia uamuzi huo kwa ajili ya kuzingatia maslahi mapana ya CHADEMA Jimbo la UKONGA.
Nawashukuru sana makamanda na marafiki wote ambao mmekuwa mkiniunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yangu nikiwa Mwenyekiti wa Jimbo la UKONGA. Sasa niwaombe tuendelee kuisupport CHADEMA na hasa Uongozi wa Mpito utakaoundwa hivi karibuni wakati taratibu za kuitisha uchaguzi mpya zikiandaliwa.
Sasa tujielekeze katika kuijenga upya kanda yetu ya Pwani iliyokuwa imedorora, ili iweze kutuunganisha na kuratibu shughuli za chama katika kanda yetu na hatimaye kanda yetu iweze kuwa kitovu na kiongozi wa mabadiliko ya uongozi katika nchi hii tunapofanya uchaguzi mkuu baadae mwaka huu 2015.
ALUTA CONTINUA...MAPAMBANO BADO YANAENDELEA
 Full story ya Mwenyekiti aliye auawa, viungo vyake vikapikwa kama mboga

Full story ya Mwenyekiti aliye auawa, viungo vyake vikapikwa kama mboga



Mwenyekiti wa Kitongoji cha Songambele, Kata ya Ilela Tarafa Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi, Richard Madirisha (31), ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na kutenganishwa na kiwiliwili na kisha kunyofolewa viungo vya mikono na miguu na sehemu za siri na kichwa chake na viungo hivyo kupikwa ndani ya safuria kama mboga.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari mauaji hayo ya kikatili na kutisha yalitokea jana saa 5.30 usiku nyumbani kwa marehemu.


Kidavashari alisema, siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe Meklina Mussa na ghafla walitokea watu watano ambao hawafahamiki na kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba.


Alisema watu hao waliodaiwa kuwa na mapanga waliingia chumbani kwa marehemu na kumlazisha mkewe ajifiche kwa kujifunika na shuka usoni.


Alisema baada ya mkewe kujifunika walianza kumchinja marehemu kwa kutumia panga huku mkewe akiwa anasikia jinsi marehemu akilia kwa uchungu.


Kidavashari alisema baada ya kumchinja walichukua kichwa na kukiweka kwenye safuria na maji na kukipika kwenye moto uliokuwa unawake nje ya nyumba ya marehemu.


Alisema kisha walirudi ndani na kunyofoa sehemu za siri, mikono na miguu na kuziweka kwenye safuria jingine kwenye moto na kutokomea kusikojulikana huku viungo hivyo vikiendelea kuchemka ndani ya safuria hizo.


Kidavashari alisema mke wa marehemu baada ya kuona watu hao wametokomea alitoka nje na kwenda kutoa taarifa kwa majirani ambao walifika kwenye eneo hilo na kukuta viongo hivyo vikiwa ninaendelea kuchemke kwenye safuria hizo huku kiwailiwili chake kikiwa ndani ya chumba chake





Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauwaji kimetokana na visa vya marehemu na mtu mmoja ambae walikuwa wakiishi nae Tabora ambae alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa amemnyanya mwanamke ambae walikuwa na mahusiano nae ya kimapenzi ambae marehemu aliamua kuhama nae kijijini hapo na kuhamia nae kijiji cha Songambele Wilaya Mlele





Kamanda Kidavashari alieleza jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limewakamata na linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo ya kikatili