
Nimepata taarifa kuwa Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Ndugu
Sospeter Muhongo amechukuwa hatua ya kujiuzulu katika nafasi hiyo.
Napenda kuchukua nafasi hii kutambua busara aliyochukua ambayo naamini
itasaidia harakati za kujenga demokrasia yenye uwajibikaji. Naamini
uamuzi wa Ndugu Muhongo umewezesha kulinda heshima ya Bunge na maazimio
yake. Kwa muda mfupi alioongoza Wizara hiyo, Ndugu Muhongo ameweza
kuongoza mabadiliko kadhaa muhimu ya kiutendaji katika wizara hiyo na
taasisi zake. Hata hivyo, nafasi ya Wizara aliyokuwa anaongoza katika
suala la Tegeta Escrow imemtia doa kubwa ambalo ilikuwa lazima
awajibike. Naamini Rais Kikwete atamteua mtu mchapakazi na makini zaidi
atakayeweza kuendeleza yale mazuri ya Ndugu Muhongo na kurekebisha
mapungufu yaliyojitokeza.
TOA MAONI YAKO HAPA
JIUNGE NASI KWA KU LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
EmoticonEmoticon