BW THOMAS NYAHENDE AMBAYE ALIKUWA NI MWENYEKITI WA JIMBO LA UKONGE
KAULI YAKE KUPITIA UKARASA WAKE WA FACEBOOK

·
Makamanda na Marafiki zangu wote,
Napenda kuwafahamisha kuwa Jana Jumamosi tarehe 24 January 2015
nimetangaza rasmi kujiuzulu nafasi yangu ya Mwenyekiti Jimbo la UKONGA.
Katika hali hiyo wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji Jimbo la UKONGA nao
wamejiuzulu ili kuungana na Mwenyekiti wao.
Hatua hiyo ngumu sana tumeifikia jana baada ya kushauriana na Mwenyekiti
wetu wa Taifa Kamanda Mbowe kufuatia hali ya sintofahamu iliyokuwepo
kwa muda mrefu baina ya Viongozi wa Jimbo la UKONGA na Mratibu wa Kanda yetu ya Pwani. Tumefikia uamuzi huo kwa ajili ya kuzingatia maslahi mapana ya CHADEMA Jimbo la UKONGA.
Nawashukuru sana makamanda na marafiki wote ambao mmekuwa mkiniunga
mkono katika utekelezaji wa majukumu yangu nikiwa Mwenyekiti wa Jimbo la
UKONGA. Sasa niwaombe tuendelee kuisupport CHADEMA na hasa Uongozi wa
Mpito utakaoundwa hivi karibuni wakati taratibu za kuitisha uchaguzi
mpya zikiandaliwa.
Sasa tujielekeze katika kuijenga upya kanda yetu ya Pwani iliyokuwa
imedorora, ili iweze kutuunganisha na kuratibu shughuli za chama katika
kanda yetu na hatimaye kanda yetu iweze kuwa kitovu na kiongozi wa
mabadiliko ya uongozi katika nchi hii tunapofanya uchaguzi mkuu baadae
mwaka huu 2015.
ALUTA CONTINUA...MAPAMBANO BADO YANAENDELEA
TOA MAONI YAKO HAPA
JIUNGE NASI KWA KU LIKE PAGE YETU HAPA CHINI
EmoticonEmoticon